
“UNADHANI wewe ni bora kuliko mimi?” Hilo ni swali la aliyekuwa mke wa msanii wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ aitwaye Fahyma almaarufu Mama Jayden akilielekeza kwa mpenzi mpya wa jamaa huyo, Paula Paul au Paula Kajala.
Mambo mengi yanazungumzwa juu ya Rayvanny kuachana na Fahyma ambaye amezaa naye mtoto mmoja wa kiume kisha kuhamishia mapenzi kwa Paula; mtoto wa mwigizaji nguli wa Bongo Movies, Kajala Masanja.Katika maelezo yake, Fahyma anamuwashia moto wa nyika Paula akimtaka asijione amepata sana kwa kutokana na baba mtoto wake, Rayvanny.“Kwa kukurahisishia, sina uhusiano na wewe tena maana umenidanganya vya kutoshaa.
“Endelea na familia yako mpya, mimi na mtoto wangu tuache hatukuhusu, kaa mbali mita 100. Zaa na hao *** (tusi),” anasema Fahyma akimweleza Rayvanny.
Hata hivyo, Fahyma hakuishia kwa Rayvanny, bali alimgeukia Paula na kumpa vidonge vyake.“Na wewe unayejiona umepata, labda nikwambie kitu, hujui chochote kile. Utaendelea kufanywa mjinga na mpumbavu mpaka kufa kwako. Malipo ni hapahapa duniani,” anasema Fahyma akimweleza Paula.
Fahyma alikuwa kila kitu kwa Rayvanny kwani wamehaso wote kabla ya jamaa huyo kuchukuliwa kwenye Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) na maisha kumnyookea ndipo akamsahau mzazi mwenzake huyo.Hii ni baada ya kuwepo kwa madai kuwa ndoa ya wawili hao ilishavunjika na ndiyo maana jamaa huyo akatua kwa Paula.
Kwa wiki kadhaa sasa, Fahyma amekuwa akitoa malalamiko yake dhidi ya Rayvanny.Fahyma anasema kwamba, ni kweli kwamba yeye na Rayvanny wameachana huku akidai kwamba msanii huyo amekuwa muongo.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram, Fahyma anasema kwamba, amesalia tu na mwanawe, Jayden, licha ya kwamba msanii huyo ni tajiri.Kupitia kwa jumbe zake, Fahyma anasema kwamba Rayvanny alikuwa amesahau familia yake na kuwa njia ya muongo ni fupi.
“Tajiri na mali yake, maskini na mwanawe malipo ni hapa duniani.”Katika ujumbe mwingine, Fahyma anasema kuwa, Rayvanny ameharibu familia yake kwa mikono yake mwenyewe na ipo siku Mungu atamkumbusha.Ujumbe wake mwingine ulisoma;
“Nimekubali kutukanwa, kubeba maumivu yote nikijua navumilia kwa mtu ambaye najua ni wa muhimu kwangu, kumbe najidanganya mwenyewe.“Imetosha, sasa siwezi tena, endelea na huo mchezo ambao hauna mwisho na sitaki.”Mama huyo aliweka wazi kwamba ametosheka kudanganywa na kwamba njia ya muongo ni fupi.Kwa upande wake, Rayvanny anakiri kutengana na Fahyma na sasa anajivinjari na Paula.
STORI: KHADIJA BAKARI, DAR