×

Mawaziri Wakutana Kujadili Michezo ya Kubahatisha

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa na katibu mkuu wa wizara hiyo, Dk Hassan Abbas wamefanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba kuhusu namna ambavyo michezo ya kubahatisha inaweza kuchangia maendeleo ya michezo na uchumi.

Taarifa ya wizara ya habari inaeleza kuwa kikao hicho kilifanyika jana Jumanne Aprili 27, 2021 ikiwa ni mikakati ya kutekeleza agizo la Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kutaka kuzalisha ajira kwa vijana kupitia michezo na sanaa kwa kuwa ni miongoni mwa sekta zinazotoa ajira kwa vijana wengi.

 

 

Leave a Comment