
RAIS wa Marekani Joe Biden, amelihutubia bunge la nchi hiyo kwa mara ya kwanza akiwa rais na kutumia sehemu ya hotuba yake kuwaonya washindani namba moja wa kibiashara wa Marekani nchi ya China.
Biden amesema kuwa Marekani haitakaa kimya wakati makampuni ya kichina yakitia usalama wa makampuni ya kimarekakani na hata ajira za raia wake.
Rais huyo amelieleza taifa lake kupitia hotuba hiyo ya bungeni kuwa katika mazungumzo yake na rais Xi Jinping wa China, ameweka wazi msimamo wake kuwa japo Marekani haitafuti mgogoro na China, lakini pia atalinda maslahi yake ya kibiashara kwa nguvu zake zote.
“Marekani itasimama kidete dhidi ya tabia zisizo za mizania katika biashara kutoka China, mambo ambayo yanawaminya wafanyakazi wa Marekani na viwanda vyao,mambo hayo ni kama kutoa ruzuku kwa viwanda vinavyoeindeshwa na serikali, wizi wa teknolijia ya kimarekani paoja na hatimiliki .”