×

Wasauzi Wampigia Simu Mo Kumuuliza Manula

TAARIFA kutoka ndani ya Simba zinasema kwamba, timu ya Mamelodi Sundowns kutoka Afrika Kusini, imelazimika kumpigia simu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’ kuangalia uwezekano wa kumsajili kipa, Aishi Manula.

 

Tangu Manula aoneshe kiwango kikubwa msimu huu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, timu kadhaa zimekuwa zikimuwania wakiwemo Wasauzi hao sambamba na Al Merrikh ya Sudan.Chanzo kutoka ndani ya Simba, kimeliambia Spoti Xtra kwamba, klabu hiyo imekuwa ikipokea ofa nyingi kutoka timu mbalimbali kuhitaji nyota wao.

 

Mtoa taarifa huyo aliongeza kwamba, wameamua kuweka kando ofa hizo wakisubiri kumaliza majukumu yao ya michuano ya kimataifa ambapo sasa wapo robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

“Ukweli uliopo juu ya Mamelodi kuitaka saini ya kipa wetu Manula ni huu, ambapo sisi kwa sasa bado tupo kwenye mashindano magumu sana, hivyo ni ngumu kuachia mchezaji asajiliwe na timu yoyote.

 

“Hivi karibuni baada ya klabu hizo kujuzwa juu ya hilo, Mamelodi Sundowns walilazimika kumpigia simu Mo wakimsisitiza wamalizane,” kilisema chanzo hicho.”

Stori: Musa Mateja, Dar es Salaam

Leave a Comment