
STORI inayo-make headlines kwa leo ni kutoka kwenye moja kati ya Big Three Music Record Label Duniani ‘Warner Music Group’ ambao wametangaza deal ya partnership na msanii wa Bongo, Diamond Platnumz pamoja na record label yake ya WCB Wasafi.

Deal ambayo itaziunganisha WCB Wasafi, Ziiki Media and Warner Music South Africa kufanya kazi kwa pamoja chini ya mwamvuli wa Warner Music ambayo itafungua milango Kidunia kwa wasanii husika kutanua wigo wa kazi zao dunia nzima.

Ukubwa wa Warner Music na mafanikio ya wasanii wenye majina makubwa wanaofanya kazi chini ya Warner unatuma matumaini kama Watanzania kuiona hatua kubwa ya Wasanii kutoka Tanzania wakifanikiwa ikiwa kipaumbele tajwa cha deal hiyo ni kuhakikisha wanapanua soko la muziki wa Diamond na WCB Wasafi kufika mbali zaidi Ulimwenguni.

Katika ku-sign deal hiyo Diamond amesema; “Ameitengeneza Wasafi kutoka chini hadi ilipo na anaamini Warner & Ziiki ni partners sahihi na anaamini watasaidia kumfikisha kwenye malengo. Anachokitazama zaidi sasa ni kuitumia vyema network ya Warner na kuhakikisha muziki wake unaufikia ulimwengu mzima.