
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, amewasihi Ndugu wa Marehemu Khatib Said Haji (Mbunge wa Konde) kuwa na subra katika kipindi hiki kigumu cha msiba wa kuondokewa na kipenzi chao.

Othman ametoa kauli hiyo baada ya shughuli za mazishi ya Mbunge huyo wa Bunge la Tanzania kupitia ACT – Wazalendo aliyezikwa Shumba Mjini, Wilaya ya Micheweni, Visiwani Pemba jana Alhamisi, Mei 20, 2021.

Mbunge wa Jimbo la Konde kwa tiketi ya ACT – Wazalendo, Khatib Said Haji amefariki dunia asubuhi ya Alhamisi Mei 20, 2021 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
