×

Rais mwinyi Afanya Uteuzi Wizara ya Habari

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amefanya Uteuzi wa Wakurugenzi katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo kama ifuatavyo:-
1) Dkt. Saleh Yussuf Mnemo ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Zanzibar (ZBC).
2) Ndugu Nasriya Mohammed Nassor ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Utumishi na Uendeshaji.
3) Ndugu Khamis Siasa Khamis ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti.
4) Ndugu Shaib Ibrahim Moh’d ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana.
5) Ndugu Salum Issa Ameir ameteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Vijana.
6) Ndugu Hassan Khatib Hassan ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo.
7) Ndugu Ameir Moh’d Makame ameteuliwa kuwa Kamishna wa Idara ya Michezo.
Uteuzi huo unaanzia leo tarehe 24 Mei, 2021.
(Mhandisi Zena A. Said).

Leave a Comment