
Mfanyabiashara Caft Kileo na Wakulima Wanne, Godfrey Samuel, Richard Andrea, Moses Paul na Benjamin Richard wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa makosa mawili ya kujihusisha na biashara ya meno ya Tembo yenye thamani ya dola za marekanai elfu kumi na tano sawa na fedha za kitanzania Milioni thelathini na nne (3,400,000).
Akiwasomea hati ya mashtaka Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simoni amedai kuwa kosa la kwanza ambalo linamhusu mshtakiwa wa kwanza na wa pili wanadaiwa kutenda kati ya Mei 5, 2021 ambapo walikuwatwa na vipande vinne vya meno ya tembo walivyokuwa wamesafirisha kutoka Mkoa wa Katavi na kukutwa navyo katika Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Katika kosa la pili linalowakabili watuhumiwa wote inadaiwa mnamo Aprili 1, 2021 katika jiji la Dar es Salama kwa nia ovu walikutwa na nyara za serikali bila kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori kinyume na sheria ya uhujumu uchumi.
Baada ya kusomewa mashtaka yao hakimu aliyesikiliza kesi hiyo, Kasian Matembele amesema washtakiwa hawaruhusiwi kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za uhujumu uchumi zinazozidi kiwango cha fedha Milioni kumi hadi kupata kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashataka ( DPP) na mahakama hiyo haina uwezo wa kutoa dhamana hadi mahakama kuu hivyo akaahirisha kesi hiyo hadi Juni 8, 2021 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.