
Mwenyekiti UBA Group na Mwanzilishi wa Taasisi ya Tony Elumelu Foundation, Tony Elumelu aliwaongoza viongozi wengine wa kimataifa wa Afrika katika kusherehekea Siku ya UBA Afrika mwaka huu. UBA imekuwa ikiadhimisha siku hii kwa miaka mingi, benki ya UBA kusherehekea siku hii kwa kupamba ofisi zao kwa mapambo ya Kiafrika na vilevile wanafanyakazi ushauri kuinga urithi wa Kiafrika kwenye maeneo kadhaa kama vile mavazi, chakula pamoja na uzuri wake.
Benki ya UBA ilianzisha siku hiyo kisha kuanzisha mazungumzo ya Siku ya Afrika ya UBA na kwa mwaka huu ilikuwa ni awamu ya tatu, UBA ukaribisha viongozi wa Afrika wanaolijua na kutambua vizuri Bara hili la Afrika na hasa kwenye maeneo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa na kwa mwaka huu viongozi walio alikwa ni Ngozi Okonjo-Iweala, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Ulimwenguni (WTO), Dk. Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), Rais wa Rwanda HE Paul Kagame na Makhtar Sop Diop, Mkurugenzi Mkuu, Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC). Kwa kuzingatia changamoto za sasa za COVID 19 imechukua hatua zaidi za usalama kwa kufanya mazungumzo haya kwa njia ya mtandao.
Akizungumza wakati wa mazungumzo hayo ambayo yalilenga zaidi athari za Covid 19, Rais Kagame alisema kuwa Covid 19 imeathiri nchi nyingi za Kiafrika kiuchumi kutokana na kufungwa kwa mipaka na kwa hivyo aliwataka viongozi wengine wa Kiafrika wajiunge pamoja na kujadili njia sahihi za kujikwamua kiuchumi. “Athari za Covid 19 zimeathiri serikali na sekta binafsi. Tunapaswa kujifunza kutokana na janga hili na kuwekeza zaidi bajeti yetu katika mfumo wetu wa kitaifa wa afya. Hili sio janga la mwisho kutoa kwa ulimwengu na inatupasa sisi kama Afrika kujiweka tayari na kujiandaa na majanga mengine yanayoweza kuja kutokea hapo kwa baadae”
Rais Kagame ameongeza, “Nadhani ni muhimu kwa viongozi wa Afrika kuja pamoja na kujadili athari za janga hili kwa pamoja kwa viongozi, tunaweza kujadili juu ya sababu za migogoro na umaskini. Sio juu ya nani anafanya hili au lile, nadhani kuheshimiana ndio njia bora ya uhusiano kati ya Afrika na ulimwengu wote, tunazungumza juu ya matatizo lukuki kwenye Bara letu la Afrika, njaa na umasikini, lakini huu sio utambulisho wetu ”.
Mwenyekiti UBA Group na Mwanzilishi wa Taasisi ya Tony Elumelu – Tony Elumelu alisema ‘Tumeona jinsi vijana wetu licha ya Covid 19 wametumia utaalam wao wa teknolojia na kuweza kujipatia kipato ili kuendesha maisha yao pamoja na kukabiliana na changamoto za ulimwengu. Kwa hivyo lazima tuhakikishe kwamba mafanikio ambayo vijana hawa wamepata hayajafutwa ’
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Shirika la Afya Ulimwenguni Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema kuwa WHO inafanya kazi siku kwa siku kuleta suluhisho la haraka kwa usambazaji wa vipimo na chanjo vya Covid. Lakini, ni wazi kuwa Afrika haiwezi kutegemea tu juu ya uingizaji wa chanjo kutoka nje ya Bara hili. Lazima tujenge uwezo sio tu kwa chanjo za Covid lakini kwa chanjo zingine na bidhaa za matibabu ‘.
Aliongeza, zaidi ya kitu kingine chochote, janga hilo limeonyesha kuwa afya sio kitu cha anasa au tu matokeo ya maendeleo bali ni haki yake kila binadamu na sharti la maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Ulimwenguni (WTO),Ngozi Okonjo Iweala, alisema kuwa ikiwa Afrika inataka kupona kutoka kwa janga la Covid, majadiliano ya kuzuia ni muhimu zaidi na nchi za Afrika zinatakiwa kupata nafasi ya kupumua ili waweze kuwekeza tu katika sekta ya afya lakini pia kwenye sekta ya uchumi na ili kuweza kupata unafuu. ‘Ni muhimu kwa ulimwengu kurekebishe ukosefu wa usawa wa chanjo na Afrika kufaidika nayo. Hatuwezi kupata uimara bila hiyo. Kwa hivyo lazima tuipiganie, iwe kwa kupata chanjo zaidi au kwa kutengeneza yetu wenyewe, alisema Iweala.