×

Usher na Jenn Watarajia Mtoto

STAA wa miondoko ya muziki wa Rnb Usher Raymond  (Usher) na mpenzi wake Jenn wanatarajia kupata mtoto wao wa pili, taarifa hii inakuja baada ya wawili hao kuweka wazi juu ya ujauzito huo usiku wa kuamkia leo.

 

Ujio wa mtoto huyo utakuwa ni wa mtoto wa tatu kwa Usher lakini wa pili na Jenn, ambapo mtoto wao wa kwanza anaitwa Sovereign Bo Raymond aliyezaliwa September 24, 2020.

 

Watoto wengine ni Naviyd na Usher V ambao aliwapata na aliyekuwa mkewe, Tameka Foster ambaye walioana 2007 na kutalakiana 2009.

 

Leave a Comment