
WAKATI ile kesi yao ya ‘washa taa’ ikiwa bado ni mbichi, mahasimu wengine wawili kunako Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’ na Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’, bado figisufigisu zinaendelea kati yao, IJUMAA limedokezwa.
Wiki kadhaa zilizopita, Harmonize au Harmo aliwafikisha Rayvanny na wenzake katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar kwa tuhuma za kusambaza video chafu iliyodaiwa ni ya kwake alipokuwa akimtongoza binti wa staa wa Bongo Movies, Kajala Masanja, Paul Paul au Paula Kajala.
HARMO AGUSA PABAYA
Habari nzito zilizolifikia Gazeti la IJUMAA zimeeleza kwamba, safari hii, Harmo amegusa pabaya baada ya kufunga safari hadi nchini Afrika Kusini (Sauzi) kwenda kumfuata msanii wa kike ambaye aliibuliwa na Rayvanny mwaka jana na Kibongobongo ni maarufu kwa jina la Mrembo wa Rayvanny.
ANAITWA BUSIMsanii huyo aliyefuatwa na Harmo ambaye ni C.E.O wa Lebo ya Konde Gang Music Worldwide anatajwa kwa jina la Busiswa Gqulu almaarufu Busi.Busi ni mwimbaji, mtunzi na mwandishi mkubwa wa mashairi nchini Afrika Kusini na amekuwa na jina kubwa kwenye ukanda huo wa Afrika Kusini.
Busi anatajwa na Shirika la Habari la CNN la Marekani kuwa ni miongoni mwa wanamuziki kumi wa kike wa kizazi hiki kutoka Bara la Afrika.Busi anawekwa kwenye kapu moja na wasanii kama Angelique Kidjo, Yemi Alade, Tiwa Savage, Sho Madjozi na wengineo.
Busi amefanya muziki kwa ukubwa duniani akiwa na mastaa wakubwa kama Beyonce kupitia projekti yake ya The Lion King, The Gift ambapo Busi alisikika kupitia wimbo uitwao The Power.Pia Busi ni mshindi wa tuzo mbalimbali kubwa za muziki ikiwa ni pamoja na za Channel O Afrika.
HARMO AMFUNGIA SAFARIKwa mujibu wa menejimenti yake, mapema wiki hii, Harmo na timu yake walimfungia safari Busi na kufanikiwa kuingia naye studio na tayari wamefanya naye wimbo matata unaokwenda kwa jina la Aya Twende.Harmo yupo mbioni kuachia album yake mpya inayo kwenda kwa jina la High School ikiwa ni albam yake ya pili baada ya ile ya Afro East aliyoiachia mwaka jana.
Kupitia Insta Story yake, Harmo amekuwa akiachia vipande vya video akiwa na mrembo huyo na kusababisha kushambuliwa na timu ya Rayvanny ambaye yupo chini ya Lebo ya Wasafi Classic Baby iliyo chini ya Diamond Platnumz.
RAYVANNY AMTAMBULISHA BONGO
Kwa mujibu wa timu ya Rayvanny, msanii huyo ndiye aliyemtambulisha Busi nchini Tanzania na Ukanda wa Afrika Mashariki kwa jumla hivyo kitendo cha Harmo kumnasa na kufanya naye kazi ni kero kwa timu ya Rayvanny au Chui.
Ili kuendelea kuuweka muziki wa juu kwenye ukanda huo wa Afrika Kusini, mapema mwaka jana, Rayvanny alifanya kolabo na mwanadada huyo maarufu pande hizo.Wimbo wa Rayvanny aliomshirikisha Busi na Baba Levo, unajulikana kwa jina la Zipo ambao mpaka sasa umetazamwa zaidi ya mara milioni 1.6 kwenye Mtandao wa YouTube.
Wimbo wa Zipo ni aina ya muziki unaochezeka ukiwa na midundo ya Afrika Kusini hivyo kuufanya wimbo huo kusikilizwa nchini humo.
HARMOKUIZIMA ZIPO?
Watu wa karibu wa Rayvanny wanadai kwamba, Harmo amefanya hivyo kwa lengo la kuizima Zipo kisha atawale yeye ukanda huo.“Kwani wasanii wako wangapi? Kwa nini aende kwa Busi?
Kama siyo Rayvanny angemjulia wapi Busi.“Alichokifanya Harmonize kwa Rayvanny ni kama alivyofanya baada ya Diamond kufanya na Koffi Olomide na yeye akafanya na Awilo Longomba; yaani kama ukimwangalia vizuri Konde Boy ni kama anataka kushika kila kitu, sasa kuna watu wanaona kama anafanya hivyo kuwadhibiti wao kama mashabiki wa Rayvanny wanavyofikiria,” kimeeleza chanzo kimoja cha karibu na Rayvanny.
Mmoja wa mameneja wa Harmo na Konde Gang, Beauty Mmary au Mjerumani alikiri Harmo kuwa nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kukamilisha albam yake hiyo ambayo kwa mujibu wa Harmo itavunja rekodi zote za albam zilizowekwa kwenye muziki wa Bongo Fleva.“Ni kweli tupo huku (Sauzi) tunakamilisha jambo letu,” alisema Beauty.
HARMO Vs RAYVANNY
Vita ya Harmo na Rayvanny imeendelea kushika kasi na kutokuwepo kwa uhusiano mzuri kwa kile
Stori; Khadija Bakari, Dar