×

Babu Tale: Neno Rais Litumike kwa Rais wa Nchi, si TFF – Video

MBUNGE wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, Hamisi Taletale amependekeza neno Rais litumike kumtaja Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan pekee.

 

Akiwa Bungeni amesema neno hilo kutumika kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) na wengineo linaishushia heshima taasisi ya Rais.

 

Ameshauri watu wapewe majina mengine ya Vyeo vyao akisema haiwezekani Rais akawa na viatu vyenye vumbi, ndio sababu yeye aliamua kujiita ‘Babu Tale’

Nchi yetu ina Rais mmoja tu Samia Suluhu, ningeomba hizi Rais wa shirikisho au TFF zitoke, wawe na vyeo vyao. Wanapunguza heshima ya neno Rais, unakuta mtu ana vumbi, Rais hawezi kuwa na kiatu kina vumbi tunatakiwa tuheshimu, ndiyo maana mimi nilijiita Babu,” Babu Tale.

Leave a Comment