
MKUU wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro leo tarehe 31.5.2021 amefanya mabadiliko madogo kwa Makamanda wa Polisi ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi baada ya Mh. Rais wa Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Samia Suluhu Hassan kumpandisha cheo Kamishna Msaidizi wa Polisi kuwa Kamishna wa Polisi na kumteua kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Camillus Wambura na Kamishna Msaidizi wa Polisi Hamad Khamis Hamad kuwa Kamishna wa Polisi na kumteua kuwa Kamishna wa Kamisheni ya Fedha na Logistiki.
1.Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Lucas Mkondya amehamishwa kutoka kuwa Kaimu Kamishna wa Fedha na Logistiki Makao Makuu ya Polisi Dodoma kuwa Mkuu wa Usalama Barabarani Tanzania.
2.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rufiji Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Onesmo Lyanga amehamishwa kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma kuchukua nafasi ya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Gilles Muroto ambaye anastaafu.
3.Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhan Ngh’anzi amehamishwa kutoka kuwa Boharia Mkuu kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza.
4.Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Mwamini Rwantale amehamishwa kutoka Kanda Maalum ya Dar es Salaam ambako alikuwa Mkuu wa Utawala na Menejimenti ya Raslimali watu kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Tazara.
5.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamishna wa Polisi (ACP) Muliro Jumanne amehamishwa kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuchukuwa nafasi iliyoachwa na Kamishna wa Polisi Camillius Wambura.
6.Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Zuberi Chembera amehamishwa kutoka Makao Makuu ya Upelelezi Dodoma kwenda Makao Makuu ya Polisi Zanzibar kuwa Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa jinai Zanzibar ambapo wanachukuwa nafasi ya Kamishna wa Polisi Hamad Khamis Hamad.
7.Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Stella Richard amehamishwa kutoka kuwa Kamanda wa Kikosi cha Polisi Tazara kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida.
SACP DAVID MISIME
MSEMAJI WA JESHI LA POLISI TANZANIA.
31.5 2021.

