Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Leo June 3,2021 amepokea ujumbe kutoka kwa Rais wa Jamuhuri ya Rwanda Paul Kagame uliowasilishwa na Mjumbe maalum na Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa wa Rwanda Dkt.Vincent Biruta
Katika ujumbe huo Rais Kagame ametuma salamu za pole kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais Rais wa Tanzania Hayati Dk. John Magufuli huku akiahidi kukuza ushirikiano kati ya Nchi hizo mbili hususani katika utekelezaji wa miradi, ukiwemo mradi wa kuzalisha umeme wa Rusumo na ujenzi wa Reli ya kisasa ya kuunganisha Jiji la Kigali na Isaka ambayo itasaidia usafirishaji.
Naye Rais Samia amemshukuru Rais Kagame kwa kutuma ujumbe huo uliojumuisha salamu za pole na pongezi sambamba na kumuhakikishia kuwa Tanzania ipo tayari kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano wake na Rwanda.
⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx