×

Wasichana Watatu Wagonganishwa Mtandaoni

KWANI mitandao ya kijamii nayo imekuwa gurio la ngono? Ukibisha utakuwa hujui kubisha.

Jamaa mmoja ametumia mtandao wa Twitter kutongoza wanawake watatu ambao ni Sharon Kiwanuka, Kevin Emmilie na Nya Lacekocot, lakini baadaye mtandao huo ukawaumbua.

Unajua ilikuwaje? Si kama unavyowafahamu tena wanawake wakipata bebi wanavyojiachia mitandaoni na picha za kichokozi ambapo mmoja wao alianza kutupia picha akiwa na mwanaume huyo wakijivinjari.

Katika pitapita ya mitandaoni mwanamke mwingine akaona ile picha, bahati nzuri jamaa alikuwa amevaa shati lilelile alilokuwa amepiga naye picha, akamfowadia mwenzake ile picha na kumwambia “dada mbona kama tumechanganywa na huyu mwanaume?”

Wakati wanaendelea kupigwa butwaa mwanamke wa tatu naye alijitokeza na kusema naye amekuwa na uhusiano na mwanaume huyo na kwamba walikutana kwenye mitandao ya kijamii jambo ambalo na wale wengine nao walikiri kwamba walikamatika kupitia mtandaoni.

STORI: RICH RICHARD | GPL

Leave a Comment