×

Serikali Yaibukia ‘Sabuni za Sumu Bongo’

JAMANI kumekucha! Ile skendo ya mjasiriamali, Andrew Mpambazi kuwa anatengeneza na kusambaza sababu za sumu imezidi kuwa nzito.

 

Taarifa za uhakika zinaeleza kuwa, serikali imeingilia kati suala hilo na kwamba imechukua sampuli kwa ajili ya uchunguzi.

 

Hali ya hewa ilianza kuchafuka wenye Jamhuri ya watu wa Twitter na kusambaa kwenye mitandao mingine ya kijamii huku ikidaiwa kuwa, sabuni aina ya Champ ni hatari kwa afya ya binadamu.

 

Imedaiwa kuwa utengenezaji wa sababu hizo hujumuisha mchanganyo wa kemikali aina ya Sodium Hydroxide ambayo inatakiwa kutumiwa kwa uangalizi makini.

 

Akizungumza na Global Publishers kwa njia ya simu mjasiriamali huyo alisema ni kweli anatumia aina hiyo ya kemikali lakini ukweli ni kwamba haina madhara kwa vile sabuni zote hutengezwa kitaalamu kwa kutumia kemikali hiyo.

 

Kuhusu kufanya kazi bila kuwa na kibari cha TBS alisema: “Mimi ni mjasiliamali mdogo nafanya kazi chini ya usimamizi wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), nafikiri unanielewa, ila watu wa serikali wamekuja wamenihoji na kuchukua sampuli, baada ya siku saba majibu yatatoka.”

@manyota_rich

 

Leave a Comment