
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Samia Suluhu Hassan anatarajia kuzungumza na wanawake zaidi ya 10,000 mkoani Dodoma jumanne June 8, 2021.
Hayo yamesemwa leo Juni 6, 2021 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.
Mtaka amesema Rais Samia atazungumza na wanawake wa mkoa huo kwa niaba ya wanawake wote nchini katika ukumbi wa Jakaya Convertion, hata hivyo, ajenda ya mazungumzo hayo haikuwekwa wazi.
Amesema wanawake kwa uwakilishi wao wa makundi kutoka wilaya za Dodoma na maeneo ya karibu wamepewa mwaliko wa kushiriki kwenye mkutano huo.