×

Rais wa Zanzibar Akutana na Viongozi Wa Dini Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Viongozi wa Dini mbalimbali Zanziubar wakiongozwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh.Saleh Omar Kabi (kulia kwa Rais) waipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu leo Juni 9, 2021.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Hussein Ali Mwinyi  leo Juni 9, 2021 amezungumza na Viongozi wa Dini mbalimbali Zanziubar wakiongozwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kabi Ikulu Zanzibar.

Umoja wa Dini Mbalimbali Zanzibar Askofu Dickson D Kaganga akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar baada ya kumaliza mazungumzo yao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar, ujumbe huo wa Viongozi wa Dini ukiongozwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar.Sheikh Saleh Omar Kabi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi, baada ya kumaliza mazungumzo na Viongozi wa Dini mbalimbali Zanzibar yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.

 

Leave a Comment