×

Rais Samia Kuboresha Maslahi ya Madaktari

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ameupongeza uongozi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), kwa kufanya kazi kubwa na kuwaahidi kwamba atahakikisha anaangalia maslahi yao vizuri.

 

Kauli hiyo ameitoa leo Juni 12, 2021, katika zoezi la  ufunguzi wa mitambo mipya ya matibabu ya moyo katika hospitali hiyo mara baada ya kuona picha zikiwaonesha madakatari wakiwa wamelala kwenye ngazi mara baada ya kumaliza kufanya upasuaji wa mgonjwa wa moyo majira ya usiku.

 

“Nimeoneshwa picha madaktari wamefanya kazi usiku wamechoka wamejibanza kwenye pembe wamelala, sasa huyo aliyekwenda kuwapiga picha sijui ni nani lakini walistahiki kulala, wamepumzika lakini alfajiri kuna operesheni zingine zinaendelea, waswahili husema mcheza kwao hutunzwa basi na serikali yenu itaangalia maslahi yenu kwakweli,” ameeleza Rais Samia.

Leave a Comment