MWANAMUZIKI Nandy amefanya balaa usiku wa kuamkia leo Juni 18, 2021 Mkoani Mwanza kwa kupiga shoo ya nguvu kwenye Tamasha lake la Nandy Festival 2021.
Nabdy ameonekana kutia huruma huku akiwataka mashabiki wake kuamini kwamba mambo yamebadilika juu ya uhusiano wake na Bill Nass (Nenga).
Ametoa kauli hiyo akiwa kwenye Tamasha lake jijini Mwanza wakati kukiwa na madai kwamba ni rasmi sasa ameachana na Nenga ambaye ameshasepa zake, lakini yeye anamuombea.
Kupitia Insta Story yake,Nandy ameandika; “Mlitegemea kuniona mimi na Nenga tukiendelea, mambo yamebadilika na simuoni tena, ila namuombea!…”
Baadhi ya mashabiki wao walitegemea kuwaona pamoja kwenye Tamasha la Nandy Festival ambalo leo ni zamu ya
Katika tamasha lake hilo Nandy, amesindikizwa na wanamuziki wengine akiwemoBaba Levo, Fid Q, Meja Kunta na wengine.
⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx