
MABINGWA wa kihistoria Tanzania bara Timu ya Yanga imeendelea kuifukuzia Simba katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara baada ya kutoka nyuma na kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mwadui FC mchezo uliopigwa jana usiku Juni 20, kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.
Mwadui FC walikuwa wa kwanza kutikisa nyavu za Yanga dakika ya 7 bao likifungwa na Aniceth Revocatus ,beki wa Yanga Bakari Mwamnyeto aliisawazishia timu yake dakika 21 akimalizia vyema mpira wa adahbu ndogo (Free kick) ya Saido Ntibazonkiza.
Yanga walikosa Penalti dakika ya 43 baada ya golikipa wa Mwadui kucheza Penalti ya Fiston Abdul Razak.
Mpaka mapumziko timu zote zilikuwa zimefungana 1-1 na kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko ya wachezaji.
Mwadui waliandika bao la pili dakika ya 65 likifungwa na yule yule Aniceth Revocatus kwa shuti kali lililomshinda Farouk Shikalo.
Dakika nne za nyongeza zilitosha kuipa Yanga ushindi wa mabao 3-2,Mabao yakifungwa na wachezaji walioingia kipindi cha pili Yacouba Songne dakika ya 90+2 na Wazir Junior dakika ya 90+3.
Kwa Matokeo hayo Yanga wanaendelea kubaki nafasi ya pili kwa Pointi 67 huku Simba wakiendelea kuongoza Ligi kwa Pointi 70 na Mwadui FC ambao wameshashuka daraja wanaendelea kukamilisha ratiba ya Ligi.