×

Chris Brown Achunguzwa na Polisi

MKALI wa muziki wa RnB Chris Brown ameripotiwa kuchunguzwa baada ya mwanamke mmoja kudai kumshambuliwa nyumbani kwake  huko Los Angeles mwishoni mwa wiki.

 

Kwa mujibu wa taarifa zilizonaswa zinadai kuwa ulitokea mzozo kati ya Breezy na mwanamke huyo ambaye jina lake halijawekwa wazi ndipo akampiga kofi kali mpaka kusababisha weave yake kutoka inagawa hakupata majeraha kando ya weave anayedaiwa kutolewa.

 

Mpaka sasa hakuna aliyekamatwa lakini mamlaka ilithibitisha kwamba polisi walifika nyumbani kwake kufuatia tukio hilo linalodaiwa baada ya kutajwa kama mtuhumiwa katika ripoti ya polisi.

Leave a Comment