Rais Samia Apokea Taarifa ya Ukaguzi wa BOT na Sensa
Global Publishers July 1, 2021 0 Comments
SHARE THIS:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akipokea Taarifa ya Ukaguzi Maalum inayohusu matumizi ya Fedha zilizotolewa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kati ya mwezi Januari na Machi mwaka huu, kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere Jijini Dodoma leo tarehe 01 Julai, 2021.
Rais Samia leo 01 Julai, 2021 Jijini Dodoma amepokea Taarifa ya Ukaguzi Maalum kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali-CAG inayohusu matumizi ya fedha zilizotolewa Benki Kuu ya Tanzania (BOT)kati ya Mwezi Januari mpaka Machi Mwaka Huu
Pia amepokea Taarifa ya maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi, inayotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka 2022, kutoka kwa Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa.
Rais Samia (kulia) akipokea Taarifa ya maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi, inayotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka 2022, kutoka kwa Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa, leo 01 Julai, 2021 Jijini Dodoma.