
Mwanadada Nandy ambaye kwa hivi sasa ni gumzo kutokana na umahiri wake usiku wa kuamkia leo alipiga bonge la shoo ndani ya Ukumbi wa Mlimani City uliopo Ubungo Dar ambapo kulikuwa uzinduzi wa simu mpya ya kijanja kabisa aina ya TECNO PHANTOM X.
Hafla ya uzinduzi huo ilipambwa na burudani mbalimbali ikiwemo ile ya mwanadada Nandy anayetisha kwenye ulimwengu wa bongo fleva.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo Meneja Masoko wa TECNO hapa nchini, William Mota alianza kutaja sifa za simu hiyo akianzia ukubwa wa memori yake GB 256 ambapo mtumiaji ataweza kuhifadhi data, mafaili picha, video na vitu vingine vingi bila kujaa haraka.
Meneja huyo amesema simu hiyo ina Ram ya GB 8 ambayo inaifanya simu hiyo kuwa na kasi ya haraka zaidi unapotaka kufungua mafaili yako au kudown load unachotaka.

Akizungumzia kioo alisema kina upana mkubwa wa urefu wa nchi 6.7 ambao unamfanya mtumiaji aweze kusoma maandishi kiurahisi, kuangalia video, picha na hata kucheza gemu kwa raha zaidi ukifurahia kioo hicho.

Kamera ya simu hiyo, Mota amesema ni ya kisasa kabisa inayomuwezesha mtumiaji kupata picha bora kabisa katika mazingira yeyote.
Ameendelea kuielezea simu hiyo kuwa katika suala la usalama unaweza kuweka finga print au password bila mtu mwingine yeyote kujua ulinzi wa simu yako.

Betri ya simu hiyo ina milium 4700 na watt 33 ambayo ukiichaji ndani ya dakika 20 unaweza kupata mpaka asilimia 20 ambazo utaweza kuzitumia kwa muda mrefu sana. Alimaliza kusema meneja huyo.
Naye Mwanamitindo na Miss Universe Tanzania, Jihan Dimack ameisifu simu hiyo ya kijanja yenye uwezo mkubwa na kuwataka wananchi kuwahi kujipatia simu hiyo ya kijanja.