Wanafunzi watatu, walinzi wanne na baadhi ya wananchi wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Geita kwa ajili ya mahojiano zaidi kufuatia matukio ya moto katika shule ya Sekondari Geita zilizoteketeza vifaa vyote vya wanafunzi wa Bweni, maabara pamoja na ghala la kuhifadhia kemikali.
Hayo yamesmwa na Mkuu wa mkoa wa Geita Rosemarry Senyamule, wakati alipoenda kutoa msaada wa magodoro, madaftari, vitabu na mashuka kwa idadi sawa ya vifaa vilivyoteketa.
“Hakuna waliobainika moja kwa moja lakini wapo waliokamtwa kwa ajili ya mahojiano na kufanyiwa uchunguzi, walinzi wamehojiwa lakini wapo baadhi ya wanafunzi na raia amabo wote wanaendelea na mahojiano, mambo yakishakamilika tutaoa taarifa zaidi,” amesema Rosemary.
Aidha, Senyamule amewatoa hofu wazazi ambao bado hawajawapeleka wanafunzi shuleni hapo kuwa shule hiyo ipo salama, isipokuwa wadau wa maendeleo waweze kujitokeza kusaidia ujenzi wa maabara ili wanafunzi wanaotarajia kufanya mtihani wasiweze kuathirika.
Nao wanafunzi shuleni hapo wamelezea hofu yao kitaaluma kufuatia ajali hizo kutokana maabara ambazo zinategemewa kwa jili ya kufanya mtihani huku wakiomba usalama kuimarishwa zaidi kuepuka matukio hayo ya moto.



