×

TRA Yakusanya Trilioni 5.15

MAMLAKA  ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kwenye kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2021/2022 imekusanya Tsh. Trilioni 5.15 sawa na ufanisi wa 94.3% ya lengo la kukusanya Tsh. Trilioni 5.46.

 

Taarifa hiyo imesema makusanyo hayo yamekua kwa 17.4% kutokana na mambo mbalimbali ambapo jambo la kwanza walilolitaja ni Watu kulipa kodi kwa hiari hususani kwenye shughuli za uchimbaji madini, mawasiliano na uchukuzi.

Leave a Comment