×

Daniel Chongolo Awataka Wana CCM Kuendelea Kuimarisha Chama

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo (kushoto) akizungumza katika mkutano wa Wanchama wa Shina no2 tawi la hasamba kitongoji cha senya (kulia) ni balozi wa Shina hilo ndg Edea Samuel (kulia) Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Songwe, Ndg. Elynico Mkola Julai 9 2021 wilayani Mbozi.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Godfrey Chongolo pamoja na wajumbe wengine wa Sekretarieti ya CCM Taifa  Julai 9, 2021 ameendelea na ziara ya kuimarisha Chama Mashinani mkoani Songwe baada ya kumaliza mkoa wa Rukwa.

Katibu Mkuu akizungumza katika kikao cha mapokezi Wilayani Momba amewakumbusha wanaCCM majukumu makubwa mawili ikiwa ni kuendelea kukijenga na kukiimarisha Chama, pamoja na kufanya kazi ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Katibu Mkuu ameongeza kuwa kuna vyama kazi zao ni kuikumbusha CCM na kuwafanya kuwa na bidii zaidi ya kuwahudumia wananchi, hivyo wanaCCM tuendelee kutimiza jukumu letu la msingi la kuongoza nchi, na wao tuwaache watimize jukumu lao.

Akianza ziara hiyo mkoani Songwe wilaya ya Mbozi, Katibu Mkuu amefanya mikutano ya Mashina na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ikwemo mradi wa Maji Kata ya Ihanda, Ujenzi wa Hospitali ya Mkoa wa Songwe pamoja kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Idiwila.

Aidha, Katibu Mkuu akiwa katika mkutano wa shina namba 02 Kata ya Hasamba, amepokea wanachama wa vyama mbalimbali vya upinzani zaidi ya 100 waliohamia CCM, wakiongozwa na Ndg. Fanuel Mkisi aliyekuwa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Vywawa kupitia CHADEMA mwaka 2020.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo akimtwisha Ndoo Kichwani ,Binti Beatrice Masasi katika Kijiji Cha Asweketa (kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Omari Mgumba mara baada ya kutembelea Mradi wa mamlaka ya Maji ya Mji Mdogo wa Vywawa wilayani mbozi.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Daniel Chongolo akisaidia shuhuli ya Ujenzi wa daraja la idiwili kwenda idunda linalojengwa kwa gharamia kiasi cha shilingi Milioni90 hadi kukamilika kwake,julai 9 2021.
Ndg. Fanuel Mkisi aliyekuwa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Vywawa kupitia CHADEMA mwaka 2020 akionesha kadi ya CCM mara baada ya kukabidhiwa na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mbunge wa Viti Maalum kutokea Mkoa wa Songwe Ndg Juliana Shonza akizungumza na Wanachama na Viongozi wa shina Namba 2 lililopo katika kitongoji cha Senya, Wilayani Mbozi.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo akizungumza na viongozi wa serikali pamoja na watumishi wa Hospitali ya rufaa ya mkoa Mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali rufaa ya mkoa inayojengwa kwa gharama za shilingi Bilioni 4.5.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Daniel Chongolo akizungumza na Wazee wa wilaya ya Mbozi jimbo la vywawa.

 

Leave a Comment