MWANAMUZIKI nyota nchini Tanzania, Ali Saleh Kiba au King Kiba ameachia kionjo cha wimbo wake mpya unaotarajiwa kuachiwa hivi karibuni.
King Kiba aliposti video fupi kwenye mitandao ya kijamii ambayo ilimuonyesha akiimba sehemu ya wimbo huo.Hata hivyo, hakufichua ni lini ataachia wimbo huo na kuwaacha mashabiki wake wakiwa na hamu sana.
King Kiba pia ameposti sehemu ya mistari iliyopo kwenye wimbo huo.Kutoka kwa video fupi aliyoposti, inaonekana kuwa wimbo hautakuwa juu ya burudani na mapenzi kama kawaida. Katika wimbo huo, King Kiba anaonekana kuwa amebadilika na kuimba kuhusu injili.
Kwenye video hiyo fupi aliyochapisha mitandaoni, King Kiba anatoa shukrani kwa Mungu kwa kuwa pamoja naye.“Walitaka niwe chini, ukanipandisha, mapenzi yako siwezi kufananisha bora nikushukuru…it’s coming get ready,” alisema King Kiba.Watumiaji wa mitandao ya kijamii walimsihi King Kiba aachie wimbo hivi karibuni wengi wakionyesha hamu na msisimko.
Tangazo la wimbo huo kuachiliwa hivi karibuni na King Kiba linakuja muda mfupi baada ya yeye kufanya kazi na mwanamuziki wa Nigeria, Rude Boy kwenye Wimbo wa Salute.Salute ilipokelewa vizuri na hadi sasa ina watazamaji takriban milioni tatu kwenye Mtandao wa YouTube.
Kabla ya hapo, King Kiba alikuwa ameachia Ndombolo akishirikiana na wanamuziki kutoka kwa Lebo ya King’s Music.
Ndombolo pia ilifanya vizuri na kuvuma mno kwenye mtandao.Ngoma hizi zinakisiwa kuwa miongoni mwa nyimbo zitakazokuwa kwenye albam yake King Kiba inayotarajiwa kutoka baadaye mwakani.
STORI: MWANDISHI WETU, DAR
