Maisha ya binadamu na viumbe wengine waliohai yanategemeana ndiyo maana tunasisitizwa kupanda miti ambayo inatupatia hewa ya oksijeni wakati huohuo binadamu na wanyama wakituo hewa ya kabonidioxide.
Katika habari hii ambayo inawza kukufanya ustaajabu ni kutokana na ng’ ombe ambaye amezaa ndama mwenye miguu miwili huko Kakamega, unaweza kufikria ni kwanamna gani binadamu anawakati mgumu kuhakikisha ndama huyu anakuwa.
Wakaazi wa kijiji cha Nang’ anda huko Navakholo, kaunti ya Kakamega wamepatwa na mshtuko baada ya ng’ ombe kuzaa ndama ambaye ana miguu miwili.
Mmiliki wa ng’ ombe huyo Zainab Makokha amelezea kwamba alikuwa amemtunza ng’ ombe huyo kabla ya kuzaa, na hakutarajia matokeo hayo.
“Nimemtunza ng’ ombe kama inavyotarajiwa kutoka kwangu nikijua siku za hivi karibuni ng’ ombe wangu ataweza kuzaa lakini nimeshangazwa na aina ya ndama aliyezaliwa,” aliiambia K24 Digital.
Kufikia sasa, ng’ ombe na ndama wako katika hali nzuri na ndama ananyonya lakini anapata shida ya kusimama wima. “Hiki ndicho kilikuwa chanzo changu cha mapato na nilikusudia kutumia maziwa hayo kusomesha watoto wangu. Kama unavyoona ndama na ng’ ombe wako katika hali nzuri, ” alithibitisha.
Wenyeji ambao walizungumza na waandishi wa habari pia walishtuka. ” Kwa kawaida tunasikia visa kama hivyo vikitangazwa kwenye redio. Lakini, hatufikiri hii ni aina ya uchawi kwani hatuna wachawi katika eneo letu, ” walisema.
Mkuu wa eneo Aggrey Oyalo ambaye alikuwa miongoni mwa watu walioshtushwa na uzao wa ng’ ombe huyo amewataka wenyeji kutumia ng’ ombe bora (dume) ili kupata ndama bora.
“Natoa wito kwa wataalam wa mifugo kutembelea nyumba hii ili kumwokoa ndama. Ninawahimiza pia wenyeji washaurie wataalam kabla ya, wakati na baada ya kupandikiza mifugo, ” alisema.
Kwa upande wake, afisa mifugo, Rajab Baraza alihusisha kesi hiyo na matumizi ya dawa za mifugo. “Visa kama hivyo vinaweza kutokea wakati mkulima anapompatia dawa ng’ ombe katika hatua za mwanzo za mimba bila maelekeo ya afisa wa mifugo, ” Rajab alisema.
