
ALIYEKUWA Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya na wenzake sita wamesomewa shtaka la uhujumu uchumi lenye makosa matano kwa madai yakuchukua Tsh milioni 90 za mfanyabiashara ili wasimchukulie hatua kwa kosa la ukwepaji wa kodi.
Ofisi ya DPP imewasilisha hati ya kuipa mamlaka mahakama hiyo,leo kupitia Wakili wa Serikali Mwandamizi,Tarsila Gervas wakati kesi hiyo ilipofikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.
Akiwasoma maelezo ya awali Wakili wa Serikali Tarsila Asenga mbele ya Hakimu Mkazi Dkt Paticia Kisinda amesema Kosa la kwanza linamhusu Lengai ole Sabaya ambapo anadaiwa kuongoza genge la uhalifu Januari 22, 2021 katika maeneo tofauti Arusha akiwa Mtumishi wa umma na kukiuka masharti ya ajira, taarifa.
Washtakiwa wote wamekana mashtaka hayo na kesi imeahirishwa hadi Septemba 16, 2021.