
Dar es Salaam. Benki ya NBC nchini Tanzania, imeendelea kuwa kinara kwa mara ya nne mfululizo katika maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam,yaliyohitimishwa jana katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam kwa kutwaa tuzo mbalimbali ikwemo ya ushindi wa kwanza katika kundi la taasisi za Fedha zilizoshiriki maonesho hayo.
Pamoja na kuwamdhamini mkuu wa Maonesho hayo benki hiyo ilikuwa mstari wa mbele katika kufanikisha ushiriki wa wadau wake mbalimbali katika maonesho hayo wakiwemo wajasiriamali, sambamba na kudhamini Kliniki ya biashara iliyoandaliwa kwaushirikiano Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE).

Akizungumza kwenyehafla ya ufungaji wa maonesho hayo Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara kwawateja wadogo na wa kati kutoka Benki ya NBC, Bw Elvis Ndunguru alisema ushirikiwa benki hiyo kwenye maonesho hayo umekuwa na tija kubwa kwa kuwa wamepatanafasi ya kuhudumia wateja wao sambamba kufungua fursa mpya za ushirikiano nataasisi mbalimbali likiwemo Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO).

“Mbali nakushirikiana na taasisi zaidi ya 16 katika kufanikisha kliniki ya biasharakwenye maonesho haya, tumefanikiwa kufungua milango na taasisi nyinginezinazohudumia wajasiriamali na wafanyabiashara wanaochipukia ikiwemo SIDO ilituweze kuona namna ambavyo tunaweza kuunganisha nguvu ili kwa pamojatuwahudumie wadau hao muhimu kwenye ukuaji wa sekta ya viwanda na biashara,’’alisema.
Aliongezakuwa wakiwa kwenye maonesho hayo benki hiyo ilipata fursa ya kupokea wagenimbalimbali wakiwemo viongozi waandamizi wa serikali akiwemo Makamu waRais Dk Phillip Mpango aliezindua maonesho hayo, mawaziri mbalimbalipamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mh Hemed Suleimani Abdulla ambaopia waliiopongeza ipongeza benki hiyo kwa namna inavyoshiriki kuwasaidiawafanyabiashara nchini.

“Kama benkitumejipanga kikamilifu kuhakikisha kwamba tunayafanyia kazi maoni yoteyaliyotolewa na viongozi waandamizi wa serikali pamoja na wateja wetuwaliotutembela lengo likiwa ni kuhakikisha kwamba tunakusanya maoniyatayatuwezesha kubuni huduma zinazoendana na matarajio yao,’’

“Benki ya NBCtumeendelea kuwa karibu na wafanyabiashara wa kati (SMEs) na ndio maanatumezidi kubuni bidhaa zinazokidhi mahitaji yao kama vile mikopo ya biladhamana kwa wazabuni na wasambazaji wa bidhaa, huduma za kidigitali zinazookoamuda pamoja na gharama nafuu zaidi za uendeshaji ili kuongeza tija kwenyebiashara zao,’’ alisema.

Akizungumziakuhusiana na ushirikiano mpya baina ya benki hiyo na taasisi yake, MkurugenziMkuu wa SIDO Mhand. Prof. Sylvester Mpanduji aliishukuru benki hiyo kwakufungua milango ya kimahusiano na taasisi hiyo huku akibainisha kuwainaonyesha wazi nia ya benki hiyo kuleta mapinduzi ya kihuduma kwa kusaidiasekta ya viwanda na biashara.

“Ushirikiano huumpya na benki ya NBC unadhihirisha nia ya benki hii katika kuinua na kuwasaidiawafanyabiashara wadogo na wa kati. SIDO tunakaribisha vyema mahusiano hayamapya na tupo tayari kushirikiana na benki kwa mustakabari mzima wa ustawi wasekta ya viwanda vidogo na wafanyabiashara nchini,’’ alisema.
