BEKI wa Real Madrid ambaye anawindwa na Manchester United, Raphael Varane, ametajwa kuwa anatafuta nyumba ya kuishi kwenye Jiji la Manchester.
Manchester United wamekuwa wakimwania mchezaji huyo kila msimu na sasa wanaonekana kuwa karibu kumchukua.
Juzi mitandao kadhaa ya England iliripoti kuwa beki huyo raia wa Ufaransa ameonekana kwenye Jiji la Manchester akiwa anatafuta nyumba ya kuishi.
Manchester United hivi karibuni ilikamilisha usajili wa mshambuliaji Jadon Sancho wa Borussia Dortmund na sasa wanataka kuhakikisha wanamchukua na beki huyo.
Mwandishi mahiri Edu Cornago, ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa mchezaji huyo na familia yake wapo nchini England kuanzia ilipomalizika michuano ya Euro.
“Varane na familia yake wapo jijini Manchester wakitafuta nyumba ya kuishi inaonekana kuwa dili lake na United lipo njiani,” alisema Edu.
