×

Mpango Awataka Watanzania Kuombea Viongozi, Taifa

MAKAMU wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango pamoja na mkewe Bi. Mbonimpawe Mpango hii leo Julai 18,2021 wameshiriki katika Ibada ya Misa Takatifu, Dominika ya 16 ya Mwaka B wa kanisa katika parokia ya Mtakatifu Maria wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, Ibada ya misa takatifu imeongozwa na Paroko wa Parokia hiyo Deusdedit Lubamba.

 

Akiwa kanisani hapo Makamu wa Rais amewaomba waumini kuendelea kuliombea taifa na viongozi ili waendelee kufanya kazi na kuwaletea maendeleo wananchi.

 

Aidha Makamu wa Rais amewasihi waumini kuendelea kufanya kazi kwa bidi na kuchukua tahadhari zote juu ya ugonjwa wa Korona.

 

Makamu wa Rais amechangia shilingi milioni moja kanisani hapo kwaajjili ya maendeleo ya kanisa hilo na sherehe za upadirisho zinazotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Leave a Comment