×

Simanzi! Mazishi ya Anna Mghwira – Video

Waziri wa TAMISEMI hapa Nchini Bi Ummy Mwalimu amewaongoza mamia ya Wananchi Wilayani Arumeru Mkoani Arusha katika kuaga Mwili pamoja na kuongoza mazishi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bi Anna Mgwira.

 

Wakati wa utoaji wa salamu za rambirambi Waziri Ummy Mwalimu ameeleza kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassani amemtuma kumuwakilisha na kuwaeleza wanachi kuwa Serikali ya imeguswa na kuumizwa na kifo cha Anna Mgwira, Hivyo Serikali itajenga Barabara kwa kiwango cha rami hadi nyumbani kwa Marehemu Anna mgwira lengo likiwa ni kuenzi kazi nzuri kwa Serikali.

 

Mazishi ya Bi, Anna Mgira yamefanyika leo Julai 26,2021 nyumbani kwake Usa River Wilayani Arumeru Mkoani Arusha na kuhuzuliwa na viongozi mba.

Leave a Comment