×

Mfanyabiashara Ndama Ahukumiwa

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu mfanyabiashara maarufu nchini, Ndama Shabani ‘Ndama mtoto wa Ng’ombe’ na mwenzake Yusuph Yusuph kulipa fidia ya dola za kimarekani 75,000 (sawa na Tsh Milioni 173.925) kwa mlalamikaji Emanuel Motilhathedi baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

 

Washtakiwa hao wanadaiwa kujipatia dola za kimarekani 150, 000 (sawa na Tsh milioni 347.850) kutoka kwa mlalamikaji huyo ambaye ni raia wa Botswana kwa madai kuwa wangemuuzia kilo 500 za dhahabu lakini hawakufanya hivyo.

 

Hukumu hiyo imetolewa jana, Jumatatu Agosti 2, 2021 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Godfrey Isaya baada ya washtakiwa hao kukiri mashtaka, kupitia majadiliano baina yao na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini ( DPP).

Leave a Comment