KLABU ya Azam FC jana jioni imefanikiwa kumsajili kipa namba moja wa klabu ya KMKM ya Zanzibar, Ahmed Ali Suleiman ‘Salula’ akisaini mkataba wa miaka miwili.
Huo unakuwa usajili wa saba wachezaji waliosajiliwa na Azam hadi hivi sasa ni Idris Mbombo (El Gouna, Misri), Paul Katema (Red Arrows, Zambia), Kenneth Muguna (Gor Mahia, Kenya), Edward Charles Manyama (Ruvu Shooting) na Rodgers Kola (Zanaco, Zambia).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na uongozi wa Azam, Salula ni mmoja wa makipa hodari, akiwa ndio tegemeo katika timu ya Taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’, anakuja kuongeza nguvu katika eneo la langoni kwenye timu yetu.
“Azam FC tunayofuraha kuwataarifu kuwa tumeingia mkataba wa miaka miwili na golikipa, tuliyemsajili kutoka KMKM ya Zanzibar ambaye ni Salula.“Golikipa huyo mwenye umbo kubwa, amesaini mkataba huo baada ya kufikia muafaka mzuri na viongozi wa Azam,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.Kipa huyo alisaini mkataba huo mbele ya
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’.