×

Mbunge Ridhiwani Kikwete Atembelea Ujenzi Bwawa la Maji, Wananchi Kuondokana na Kero ya Maji

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete akizungumza na baadhi ya wananchi wa Vitongoji mbalimbali vya jimbo lake kuhusiana na mradi huo mkubwa ambao ukikamilika utawaweza kupunguza adha ya maji katika maeneo hayo.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete (mwenye fulana ya kijana katikati) sambamba na wanachi wa maeneo hayo wakishuhudia eneo lililoandaliwa kwa ajili ya mradi.

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete ametembelea eneo la Ujenzi wa Mradi wa Bwawa Kubwa la Maji litakalogharimu Shilingi Milioni 900 huko Mjembe, Kwamduma linalojengwa na Wakala wa Maji Vijijini-RUWASA ambalo ujenzi wake ukikamilika utaweza kupunguza adha ya maji kwa wakazi wanaozungukwa na eneo hilo la mradi.

 

“Nimetembelea kuona maendeleo ya Ujenzi wa Mradi wa Bwawa Kubwa la Maji litakalogharimu Shilingi Milioni 900 huko Mjembe, Kwamduma linalojengwa na Wakala wa Maji Vijijini-RUWASA, Litakapokamilika litapeleka maji kwa Vitongojj vyote kwa kijiji cha Kwamduma. Pia nimeongea na wananchi kuwaasa kujikinga kupambana na gonjwa la Korona na kuwashauri kwenda kuchanja. #AsanteSerikali #KaziInaendelea” alisema.

Leave a Comment