
Ofisi ya Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania imeeleza na kusikitishwa na kulaani kitendo cha Muunguzi msajiliwa Scholastica Kanje anayefanya kazi Hospitali ya Rufaa ta Mount Meru mkoani Arusha kwa kufanya mizaha katika jambo la Kitaifa la utoaji chanjo ya ugonjwa hatari wa UVIKO 19 ambapo aliigiza kumchoma mteja sindano na ili hali hakumchoma na kusambaza katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
Baraza la Uuguzi na Ukunga ni mamlaka ya kisheria inayosimamia huduma za uuguzuzi na ukunga chini ya Sheria namba 1 ya mwaka 2010 (The Nursing and Midewifery Act 2010). Hii inaweza kuleta upotoshaji mkubwa na kuzua taharuki kwa wananchi.

Ofisi ya Rais – TAMISEMI imetangaza kusikitishwa na kitendo cha watumishi wawili (2) Mwl. Omary Abdallahemed Kwesiga Mkuu wa Idara Elimu Msingi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha na Scolastica L. Kanje Afisa Muuguzi Msaidizi hospitali ya Mkoa wa Arusha kufanya igizo kwenye zoezi la chanjo ya COVID-19 kinyume cha Taratibu na kanuni za Utoaji wa Chanjo hivyo kuleta sitofahamu kwa wananchi kuhusu zoezi la Chanjo linaloendelea nchini kote.
Kufuatia hali hiyo, Waziri wa Nchi, OR-TAMISEMI, Mhe. Ummy Mwalimu amemuagiza Katibu Mkuu OR-TAMISEMI kumsimamisha kazi Mwl. Omary Abdallahemed Kwesiga Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi Halmashauri ya Jiji la Arusha. Aidha, ameagiza Scolastica L. Kanje Afisa Muuguzi Msaidizi apelekwe kwenye Baraza la Wauguzi na Wakunga kwa hatua zaidi.
