
RASMI Kampuni ya Jan International kupitia Mkurugenzi wake, Jan Mohamed Kishki leo Agosti 6, 2021 imeandikishana saini na Azam Tv mikataba ya gari mpya aina ya Toyota Crown kwa ajili ya mshindi wa pambano kati ya Twaha Kiduku na Dullah Mbabe.
Katika tukio hilo ambalo limefanyika kwenye ofisi za Jan International zilizopo Namanga jijini Dar tayari kwa pambano Usiku wa Deni ambalo litawakutanisha mabondia hao huku likipangwa kupigwa Agosti 20, mwaka huu kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar.

Pambano hilo la linatarajia kuchezwa kwa raundi kumi katika uzito wa kati limedhaminiwa na Spoti Xtra, +255 Global Radio, Jembe Energy, Azam Tv, Kebbys Hotel, Dash Communication, Asas, Smart Gin, Creative Bee, Afya, Good Hope Laboratory na K4S Security.

Akizungumza mara baada ya tukio hilo, meneja michezo wa Azam Tv, Tinna Corroso alisema kuwa ameishukuru kampuni hiyo kwa kuweza kutoa zawadi hiyo kubwa kwa bondia atakayefanikiwa kuibuka mshindi kwenye pambano hilo ambalo limekuwa na upinzani mkubwa.
Stori na Picha: Ibrahim Mussa