
USAJILI: Jorge, baba wa mshambuliaji nyota Argentina na Barcelona, leo Jumanne, Agosti 10, 2021, ameviambia vyombo vya habari nchini Hispania kuwa mwanae anajiunga na Paris Saint Germain (PSG).

Messi aliondoka uwanja wa ndege wa El Prat jijini Barcelona leo Jumanne asubuhi 🗼 kuelekea Paris kwa ajili ya kusaini mkataba mpya na vigogo hao wa Ufaransa.

Lionel Messi amekubali kusaini mkataba wa miaka 2️⃣ na PSG ya Ufaransa 🇫🇷 kikiwa na kipengele cha kuongeza hadi Juni 2024.
Messi mwenye umri wa miaka 34 atalipwa Paundi milioni 25 kwa mwaka (sawa na Tsh bilioni 80.362) baada ya kukatwa kodi, pia atalamba bonsai kama zote.

Hii imekuja baada ya kuachana na klabu yake ya Barcelona aliyoitumikia kwa miaka 18 kutokana na mkataba wake wa miaka mitano kushindikana kutokana na sheria za La Liga licha ya Messi kukubali kukatwa asilimia 50 ya mshahara wake.

Messi anakwenda kuungana na swahiba wake, Neymar Jr aliyekuwa naye Barca miaka michache iliyopita, Pamoja na Kylian Mbappe na Mu-Argentina mwenzake, Angel Di Maria katika kikosi hicho kinachonolewa na Mauricio Pochettino.
