
KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes leo Jumanne, Agosti 10, 2021 kimekwea pipa kuelekea nchini Morocco kwa kupitia Dubai.

Kikosi kitafika Dubai leo usiku na kesho asubuhi kitaondoka Dubai kwenda Casablanca, Morocco.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho wanajipanga kwa ajili ya msimu wa 2021/22.

Miongoni mwa wachezaji waliokwea pipa ni pamoja na Bernard Morrison, Meddie Kagere , Mohamed Hussein, Erasto Nyoni.

Pia kiungo wao mkabaji, Jonas Mkude ambaye alikuwa amesimamishwa kwa muda usiojulikana kutokana na masuala ya nidhamu.

Pia Perfect Chikwenda naye yupo katika kikosi hicho kitakachoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.


View this post on Instagram