
Dar es Salaam, Agost 11, 2021. Kampuni inayoongoza kwa maisha ya kidijitali, Tigo Tanzania, imeshirikiana na kampuni ya Sanlam, kuanzisha bima ya simu janja (Smartphones).
Huduma hii ni kwa simu mpya zinazonunuliwa katika maduka ya Tigo kote nchini. Mpango huu ni kwaajili ya simu zinazopotea, kuharibika kwa bahati mbaya au kuibiwa.

Akizungumzia ushirikiano huo, Mkuu wa Maduka na Bidhaa zaTigo, Mkumbo Myonga alisema, “Katika ulimwengu ambapo simu janja zimekuwa muhimu sana kwa watu wengi ambao huzitegemea kuwasiliana na dunia kupitia mitandao ya kijamii, huku wengine wakizitumia kama ofisi zao za kazi, ushirikiano huu na Sanlam utawapa bima wamiliki wa simu za mkononi endapo simu zao zitapotea au kuharibika”.

“Mara baada ya wateja kununua simu kutoka kwenye maduka yetu, mbali na dhamana (warranty) ya kawaida, tunashauri wakatie bima simu janja zao mpya.

Mpango huu unakidhi haja za wateja wetu, hususani wanaotaka kulinda simu zao zinazoharibika au kupasuka kwa bahati mbaya.

Muda wa bima utakuwa ni miezi 12 (mwaka mmoja) ambapo mmiliki wa simu atatakiwa kulipa asilimia 5 ya jumla ya gharama ya kununulia simu yake ya mkononi kama malipo ya bima.” Alieleza Mkumbo.
Wateja wanaweza kupata bima ya simu janja kwa kutembelea maduka ya Tigo yaliyopo nchi nzima. Kwa maelezo zaidi, wateja wanaweza kutembelea tovuti ya www.tigo.co.tz au kupiga simu bure kwenda namba 0800 714 447.
Akiwa katika tukio la uzinduzi, Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa Sanlam, Geofray Masige alisema, mpango huu wa bima, utahakikisha kuwa wateja wa Tigo wanatengenezewa au kurudishiwa simu zao haraka baada ya kuharibika au kupotea ndani ya muda uliowekwa.
“Simu janja sasa imekuwa ni sehemu ya maisha ya kila siku ya wanadamu. Ukiachia mbali gharama halisi ya kununulia, kifaa hiki kina thamani kubwa kwa mtumiaji wake na hofu ya kupoteza ni kubwa kwa watu wengi, lakini kwa hili Sanlam na Tigo tumeleta suluhisho,” alisema.
Masige aliongeza kuwa, mpango huu wa bima ya simu za mkononi ni nafuu sana na kujiandikisha ni rahisi sana, maana hakuna kutumia makaratasi, bali taarifa zote za mteja zitahifadhiwa kidijitali.
Mteja atalipwa madai yake ya fidia ndani ya siku 14 huku madai ya simu iliyoibiwa yakichukua mpaka siku 7 tu baada ya kuwasilisha nyaraka zote zinazohitajika.
Taarifa zaidi pia zinapatikana kupitia ofisi zote za Tigo na Sanlam jijini Mwanza, Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Mbeya.
Kuhusu Tigo:
Tigo Tanzania ni kampuni inayoongoza kwa maisha ya kidijitali. Ilianzishwa mwaka 1994 ikiwa mtandao wa kwanza Tanzania wa simu za mkononi.
Ni kampuni ya mawasiliano yenye ubunifu mkubwa nchini na ambayo inatoa huduma zinazolenga kuleta mageuzi ya kidijitali katika maisha ya watanzania.
Inatoa huduma mbalimbali kuanzia huduma ya sauti, ujumbe mfupi, intaneti yenye kasi na huduma za kifedha za kwenye mitandao ya simu za mkononi, Tigo imeanzisha ubunifu kama vile Facebook ya Kiswahili, Kiunga cha Tigo Pesa kwa watumiaji wa simu za Android & iOS, Tigo Music (Deezer) na huduma ya kwanza Afrika Mashariki kutuma fedha kwa njia ya simu za mikononi nje ya nchi yenye uwezo wa kubadili sarafu ya nchi husika
Kwa taarifa zaidi tembelea: www.tigo.co.tz au wasiliana na:
WoindeShisael–Meneja Mawasiliano, [email protected]
Kuhusu Sanlam
Sanlam ni kampuni inayoongoza kwa huduma mbalimbali za kifedha ndani ya Afrika, iliyoorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Johannesburg na Namibia.
Sanlam ilianzishwa mwaka 1918 kama kampuni ya bima ya maisha. Leo, kampuni hii inaendesha biashara zake katika nchi 33 Barani Afrika, na pia Marekani, Malaysia, Uingereza, India, na Australia.
Kampuni ya Sanlam General Insurance Tanzania imekuwa ikifanya kazi tangu 1998 na inatoa huduma zote za bidhaa za bima kwa wateja binafsi na kampuni. Bidhaa binafsi zinazotolewa ni pamoja na bima ya magari, moto, shughuli za baharini, uhandisi nk.