
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linawashikilia watu sita kwa tuhuma za kuwashambulia na kuwarekodi video za utupu watu wawili waliokuwa faragha na kisha kuzisambaza mitandaoni kwa madai ya kwamba wamewafumania.
Hatua hiyo imekuja kufuatia agizo la Waziri wa Mambo ya Ndani George Simbachawene, alilolitoa Agosti 6, 2021, Jijini Dar es Salaam, baada ya kuona video inayosambaa mitandaoni ikionesha mwanamke na mwanaume waliokuwa faragha wakidhalilishwa kwa kupigwa wakiwa watupu.
Taarifa ya kukamatwa kwao imetolewa na Kamanda wa Kanda hiyo Muliro Jumanne, Watuhumiwa hao ni :-
1. Singiba Buchadi (42), Fundi umeme, Mkazi wa Kongowe Mwisho Mkuranga.
2. Dephina Buchadi (42),Mfanyabiashara, Mkazi wa Kongowe Mkuranga.
3. Doratea Mathayo (39), Mkazi wa Kongowe Mwisho
4. Wilbard Teobard (55), Mkazi wa Kongowe.
5. Albert Buchadi (30), Mkazi wa Kongowe.
6. Valenzi Silvester (40),Mkazi wa Kongowe.
Vitendo vya kikatili walivyovifanya watuhumiwa hao ni pamoja na kutoa adhabu wakati wao sio Mahakimu au Majaji. Vitendo hivyo havikubaliki kisheria katika nchi inayofuata mfumo wa utawala wa sheria na kwa sababu hizo watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo na kwamba ukatili walioufanya ni wakutoa adhabu ilhali wao si Mahakimu wala Majaji.
“Vitendo vya kikatili walivyovifanya Watuhumiwa hao ni pamoja na kutoa adhabu wakati wao si Mahakimu au Majaji, vitendo hivyo havikubaliki kisheria katika Nchi inayofuata mfumo wa utawala wa sheria na kwa sababu hizo watafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo,” amesema Kamanda Muliro.