
Rwanda imetangaza kusitisha safari zake za ndege kwenda Johannesburg na Cape Town South Africa, Lusaka Zambia na Harare Zimbabwe na kurejesha masharti ya karantini ya siku saba kwa wote wanaotoka kwenye Nchi hizi.
Rwanda imeungana na Nchi nyingine zaidi ya kumi na tano zikiwemo Uingereza na Marekani kuzuia Wasafiri kutoka Nchi hizo kutokana na kirusi kipya hatari cha corona ambacho kimegundulika South Africa hivi karibuni.