×

Mwanafyale, Mchapeni Nusura Wazichape Kavukavu Msamvu

MABONDIA Danny Mwanafyale na Joseph Mchapeni nusura jana wazichape kavukavu kabla ya kupanda ulingoni leo Jumamosi kwenye pambano Face Off ya Twaha Kiduku na Dullah Mbabe.

 

 

Mabondia hao wanatarajia kupanda ulingoni leo  Jumamosi kwenye Ukumbi wa F2, Florida Msamvu kwa kiingilio cha Sh 5000 kwa watu maalum na Sh 2000 kwa VIP chini ya udhamini wa Global Tv Online, Dash Communication, Smart Gin, Creative Bee na Gazeti la Championi.

 

 

Katika tukio hilo la uzito ambalo limefanyika kwenye kituo kikuu cha mabasi Msamvu hapa Morogoro, Mwanafyale na Mchapeni ndiyo walikuwa gumzo kabla ya pambano huku Mwanafyale alikuwa makini wakati wa kupima uzito ili asiruhusu kupigwa ngumi kama ilivyotokea kwenye kutangaza pambano hilo.

Wengine waliopima uzito ni Mohamed Jailan vs Kanda Kabongo, Mwinyi Mzengela vs Ramadhani Mbengu, Juma Misumali vs Abdul Ubaya, Karim Ndonga vs Omari Athumani, Ally Jent vs Nassor Madimba.

 

Pia Babuu Luda na Ayoub Mwankina, Abdul Malunde Issa Chikawe, Pascal Manyota vs Pascal  Manyota na Leonard Dedani.

 

 

Na Ibrahim Mussa, Morogoro

Leave a Comment