
Dar es Salaam: 13 Agosti, 2021. GSM Home – kampuni inayoongoza kwa mauzo ya samani bora za majumbani na maofisini – kuanzia leo inawawezesha Watanzania wote kununua bidhaa zenye ubora wa kimataifa kupitia mfumo wa kuwekesha /kudunduliza malipo Lipa Kidogo Kidogo, huku wakifurahia ofa nyingine murwa kutoka GSM.
Akizindua huduma hiyo mpya ya Layby au ‘Lipa Kidogo Kidogo’ jijini Dar es Salaam jana, Afisa Mkuu wa Biashara wa makampuni ya GSM, Bw Allan Chonjo alisema kuwa mfumo huo wa kuwekesha ‘Lipa Kidogo Kidogo’ ni suluhisho sahihi kwa mahitaji ya wateja ambao wanataka bidhaa za kipekee za GSM kwa malipo nafuu zaidi, bila makato riba wala gharama ya maombi ya ziada.

“Daima GSM tunawasikiliza na kuwajali wateja wetu. Ndio maana leo tunaanzisha mfumo mpya utakaowezesha kuchagua na kulipia bidhaa na samani zetu za majumbani na maofisini kwa mfumo wa kudunduliza/ kuwekesha ‘Lipa Kidogo Kidogo,’.” alibainisha.
Kupitia mfumo huu, mteja anachagua bidhaa anayohitaji na kuingia katika makubaliano yanayompa uhuru wa kulipia kianzio cha asilimia 20, na kisha kama thamani ya bidhaa husika ni kati ya shilingi milioni moja na milioni tatu, atalipa salio ndani ya miezi mitatu, huku ikiwa thamani ya bidhaa ni zaidi ya milioni 3 na Mil 4 hadi Mil 6 atalipa salio ndani ya miezi 6.
“Kwanza na kukamilisha malipo ya bidhaa aliyochagua kwa kipindi maalum na kwa bei ile ile, kuendana na makubaliano yetu.
Sisi GSM Home tutamhifadhia bidhaa alizochagua kwa uhakika na usalama hadi pale atakapokamilisha malipo yako.
Sahau yale maumivu ya kukipenda kitu na wakati bado unakitafuta pesa ya kukinunua, unakuta kimenunuliwa tayari, na sisi humkabidhi mzigo wake bila makato mengine yoyote ya ongezeko la thamani au ya kuhifadhi bidhaa husika,” aliongeza
Kupitia mfumo huu mpya, wateja wa GSM Home watakaochagua bidhaa yoyote yenye thamani kati ya shilingi milioni moja hadi milioni tatu wataruhusiwa kuingia makubaliano na kulipia kianzio sawa na asilimia 20 ya thamani ya bidhaa husika.
Wateja hao kisha watakamilisha malipo yaliyobakia kwa mfumo wa kudunduliza kwa muda usiozidi miezi mitatu mfululizo, kabla ya kukabidhiwa kile walichonunua.
Nao wateja watakaonunua bidhaa zenye thamani zaidi ya shilingi milioni tatu, vilevile wanaweza kuingia makubaliano ya kuwekesha asilimia 20 ya thamani ya bidhaa waliyochagua, na kisha kukamilisha malipo yaliyobakia kwa kulipia kwa awamu ndani ya muda usiozidi miezi sita kulingana na makubaliano waliyoingia.
Vilevile, kuanzia leo tarehe Tar 13 Agosti hadi tarehe mpaka Tar 15 Septemba, GSM Home wanaendesha promosheni kabambe inayowazawadia wateja wote watakaotembelea maduka yao na kufanya manunuzi ya shilingi laki tano, vocha bure itakayowawezesha kufanya manunuzi zaidi ya shilingi laki moja.
Itakayowawezesha wateja watakaofanya manunuzi ya Tsh 500,000/= na zaidi kuzawadiwa vocha ya Tsh 100,000/= wanayoweza kuitumia kufanya manunuzi zaidi kwenye maduka yote ya GSM – (Max, Babyshop, Splash, Shoexpress, Anta Sports na Homebox).
“Tunawakaribisha Watanzania wote kutembelea maduka yetu ya GSM Home yaliyopo Dar es Salaam, Dodoma, Arusha na Mwanza ili wafurahie ofa hizi kabambe kutoka GSM,” Allan alisema.
Akizungumzia mfumo huo mpya wa kuwekesha/kudunduliza ‘Lipa Kidogo Kidogo’ kutokana na ofa hiyo kutoka GSM Home, mteja aliyetembelea duka la GSM Home – Nuru Bakari aliwashukuru GSM kwa kuleta usawa katika manunuzi na kuongeza alisema kuwa mfumo huo ni rafiki sana kwa wateja.
“Mfumo huu wa malipo ya kudunduliza utainua maisha ya Watanzania kwa sababu sasa nina uwezo wa kununua bidhaa murwa za GSM na kulipia taratibu bila kuumiza sana mifuko yangu, na kuzawadiwa kwa kufanya manunuzi yangu katika maduka yao ‘Lipa Kidogo Kidogo’ utawasaidia sana hata Watanzania wasioweza kumudu gharama moja kwa moja kwa kuwapa muda wa kujipanga na kuanza kulipia kidogo kidogo huku wakiwa na uhakika wa kuhifadhiwa bidhaa walizozipenda na kuzichagua.
“Inafurahisha kuwa unalipia bidhaa tena bila kulipia riba au gharama za maombi. “Asanteni GSM kwa kuleta usawa kwenye manunuzi ya GSM” alisema.