
WATU 304 wamefariki baada ya tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.2 katika vipimo vya Ritcher jana Agosti 14, kugonga magharibi mwa Haiti na kuharibu majengo ikiwemo makanisa na hoteli, waziri mkuu amesema ulikuwa “uharibifu mkubwa ” na kutangaza mwezi mmoja wa hali ya hatari.
Mwaka 2010 tetemeko la ardhi lilokumba Haiti liliwaua watu zaidi ya 200,000 na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundo mbinu na uchumi.
Tetemeko hilo limetokea kukiwa na mzozo wa kisiasa nchini, kufuatia kuawa kwa Rais Jovenel Moïse mwezi uliopita.
Rais Joe Biden ameamuru Marekani ”kuingilia kati mara moja” kusaidia nchi hiyo na kusema kwamba shirika la USAID litasaidia katika juhudi za “kutathmini uharibifu na kuwaokoa wale waliojeruhiwa na wale ambao watalazimika kujenga tena”.