
Mshtakiwa namba moja katika kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amesema Polisi na waendesha Mashtaka wamedanganywa kuhusu shitaka lililopo Mahakamani na limetengenezwa kisiasa sababu ya chuki hivyo ameomba Mahakama imuachie huru.
Akiongozwa na Wakili wa utetezi Moses Muhuna wakati akijitetea mbele ya Hakimu Mfawidhi Odira Amworo huku akilengwa na machozi, Sabaya amesema shitaka hilo limetengenezwa kutokana na siasa zilizopo kati ya Mkoa wa Arusha na Hai.
Sabaya amesema kwa wiki tatu akiwa DC watu walitaka kumuua na hakuna asiyejua, vilevile akiongea huku akitokwa machozi amesema mashahidi wameshindwa kuthibitisha kilichotokea huku vyote vilivyotajwa Mahakamani hajavifanya hivyo akaomba aachiwe huru.
”Shitaka nililotengezewa Polisi wamedanganywa waendesha mashtaka wamedanganywa kwa misingi ya Giriba na Chuki sababu za kisiasa na niaina ya Siasa za Arusha na Hai,” amesema Sabaya.
Sabaya aliileza mahakama kuwa anamshukuru Mungu kwa kuwa anaendelea kuishi kwa kuwa kabla ya kesi kunamambo mengine makwabwa yalikuwa yamepangwa dhidi yake Sabaya machozi yakashindwa uwezo wa mcho kuyazuia huku machozi yakimdoka usoni akiuinamisha chini machozi yakichuruzika moja kwa moja kwenye barakoa nyeupe aliyoivaa mdomoni akiongea kwa huzuni na kwikwi.
“Kwa wiki 3 nilikuwa mkimbizi ndani ya nchi yangu kwa mara mbili watu walifanyamajaribio ya kutaka kuniua ndania ya wilaya yangu Hakuna viongozi wasiojua hata vyombo vyote vya ulinzi na usalama na mamlka inajua.
“Na kwa vyovyote Mhe. Hakimu mimi malipo yangu yasingeweza kuwa hayo yakuambiwa nimeiba mali ya mmachinga elfu 35 wakati mimi niliwahi kuwapigania mali zao zikarudishwa hayawezi kuwa malipo hayo,” amesema Sabaya.
Mbele ya Mahakama shitaka la tatu Sabaya ambaye alidaiwa kabla ya kumuibia Hans simu yake alimpiga na kuchukua shilingi elfu 35 na kumtishia kwa Bunduki.
Sabaya amesema, shahidi huyo anaedaiwa kutendewa hayo alifika mahakamani akiwa shahidi wa tatu katika maelezo yake hapa mahakamani hakuna sehehemu yoyote aliyosema aliwahi kufungwa pingu na kama ailitishiwa na Bunduki kabla na baada ya kuibiwa fedha.
Alisema hapa mahakamani hamjui aliyempekua maungoni nani aliyemuobia hiyo simu Sabaya Mbele ya Mahakama aliieleza kua Shahidi huyo namba tatu anaedaiwa kupigwa na kuibiwa simu na fedha na upande wa Jamuhuri Alishindwa kuleta vielelezo vya ushahidi mahakamani wakati akitoa ushahidi wake.