×

RC Makalla Apokea Mwenge Wa Uhuru, Miradi Zaidi Ya 46 Kukaguliwa

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla akiwa na Mwenge wa Uhuru 2021 baada ya kuupokea.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Aboubakar Kunenge (kushoto) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru 2021 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla.
Mkimbiza Mbio za Mwenge wa Uhuru 2021 kitaifa (kulia) akizungumza jambo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar.
Taswira ilivyoonekana wakati wa kuupokea Mwenge wa Uhuru ukitokea katika Mkoa wa Pwani.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo amepokea mbio maalum za Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa Ndege wa Mwl JK Nyerere Terminal 1 ukitokea Mkoa wa Pwani.

Akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mhe Abubakar Kunenge Mkuu wa Pwani , Mhe Amos Makalla amesema Mwenge wa Uhuru utakimbizwa umbali wa KM 355.6 ukizindua na kuweka jiwe la msingi katika miradi ya Maendeleo ipatayo 46 iliyokamilika na iliyoko katika hatua za utekelezaji yenye thamani zaidi ya Bilioni 105.

Baada ya kukimbizwa katika Wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam, Agosti 23, 2021 Mwenge wa Uhuru utakabidhiwa katika Mkoa wa Lindi.

Aidha Mhe Mkuu wa Mkoa amekabidhi Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Ilala tayari kwa kuanza kukimbizwa ndani ya Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam.

 

Imetolewa na: Kitengo cha Habari na Uhusiano Ofisi ya Mkoa wa Dar es Salaam

Leave a Comment