×

Breaking: Watumishi Watano wa TRA Wafariki kwa Ajali

Watumishi watano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kikosi kazi cha Fast Track wamefariki kwa ajali katika eneo la Hanseketwa – Old Vwawa wakati wakiwa katika majukumu yao ya kazi wakifukuzana na gari iliyodhaniwa kubeba magendo.

Ajali hiyo imetokea baada ya gari walilokuwa wamepanda aina ya Toyota Land Cruiser kugongwa kwa nyuma na lori la mizigo aina ya Fuso.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe ACP Janeth Magomi Kamanda Magomi amethibitisha na kusema kuwa ajali hiyo imetokea leo Agosti 23, 2021 majira saa 11 alfajiri katika eneo la Hanseketwa – Old Vwawa lililopo wilayani Mbozi, Songwe.

Kamanda amesema kwamba ajali hiyo imesababisha vifo vya wafanyakazi wanne wa TRA mkoa wa Mbeya na mmoja wa TRA Tunduma, ambapo wote walikuwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya doria mipakani kwa lengo la kukomesha biashara ya magendo.

 

Taarifa za awali zinadai kuwa Watumishi hao walikuwa kazini, ambapo walikuwa wakitumia gari hiyo kufukuza gari nyingine iliyohisiwa kubeba bidhaa za magendo. Miili ya marehemu hao wote imehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Songwe.

ACP Janeth amesema polisi wameanza uchunguzi wa ajali hiyo; “Wate walikua wakitekeleza majukumu yao ya doria mipakani ambapo walishuku gari moja kuwa inaweza kuwa ikisafirisha magendo,” alisema.

 

Hadi sasa TRA haijatoa tamko lolote kuhusiana na ajali hiyo. Mashuhuda wa ajali hiyo wamenyoshea kidole mwendokasi na kukosa umakini wa madreva kama chanzo cha ajali hiyo.

 

Leave a Comment